Kadi moja ya harusi: inafika kwa kila mgeni, inajibu, inachangia, inaingia mlangoni.
WhatsApp, SMS au karatasi — kila mgeni anapata kadi yake yenye QR na namba. Hata bila smartphone, hata bila mtandao.
Harusi Pass ni nini?
Harusi Pass ni huduma ya Kitanzania ya kadi za mwaliko za mtandaoni. Kila mgeni anapata kadi yake kwa WhatsApp, SMS au karatasi, ikiwa na QR na namba fupi. Kamati inaona nani amejibu, nani amechangia, na nani ameingia langoni, hata mtandao ukikatika.
Jinsi inavyofanya kazi
- 1
Ingiza wageni
Bandika orodha, pakia CSV au chagua kutoka kwenye anwani za simu. Tunasafisha namba zote.
- 2
Tuma kadi
WhatsApp kwa wenye smartphone, SMS kwa wengine, na PDF ya kuchapisha kwa wazee.
- 3
Wageni wajibu & walipe
Mgeni anathibitisha kuhudhuria na kulipa mchango kwa simu — bila kuingia kwenye akaunti.
- 4
Wafike langoni
Kamati inaskani QR au kuandika namba. Inafanya kazi hata mtandao ukikatika.
Kwa harusi, send-off, uchumba na zaidi
Kwa wageni wasio na smartphone
Kila mgeni anapata namba fupi kama KH-4826 kwenye SMS au kadi ya karatasi. Mlangoni, kamati inaitafuta kwa namba, jina au tarakimu nne za mwisho za simu.
- SMS inayosomeka kwenye simu yoyote
- Kadi ya karatasi yenye QR na namba
- Mlangoni: QR, namba au jina
Imani kwanza
Mtumaji anaonekana
Kila kadi inaonyesha jina la kamati, simu yao na kiungo rasmi.
Hakuna viungo vya ulaghai
Hatuombi nenosiri wala PIN, na hatutumi viambatisho au programu.
Data zako ni zako
Namba za wageni zinatumika kwa tukio lako tu. Unaweza kuzipakua au kuzifuta wakati wowote.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Je, kadi ya karatasi bado inawezekana?
Ndiyo. Unapakua PDF ya kadi zote — kila moja ina QR na namba ya mgeni — na kuchapisha popote.
Mgeni asiye na smartphone atapataje kadi?
Atapokea SMS yenye kiungo kifupi na namba ya kadi. Mlangoni anataja namba tu.
Itakuwaje mtandao ukikatika siku ya harusi?
Programu ya mlangoni inahakiki QR bila mtandao na kusawazisha baadaye. Kadi ya mgeni pia inaonekana bila mtandao baada ya kufunguliwa mara ya kwanza.
Michango inalipwaje?
Mgeni analipa kwa M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money au HaloPesa kutoka kwenye kadi yake. Kamati inaweza pia kurekodi malipo ya taslimu.
Mtu akipiga picha ya QR ya mwingine?
Kila QR ni ya mgeni mmoja na inaweza kuingia mara moja. Ikiskaniwa mara ya pili, kamati inaona ni nani aliingia na saa ngapi.
Gharama ni kiasi gani?
Wakati wa majaribio ni bure. Gharama za SMS zinaonyeshwa kabla ya kutuma.